Mfumo wa utoaji siri – Maelezo ya uhifadhi wa data ya Ujerumani
Tunazingatia zaidi masuala ya ulinzi na usiri wa data na tunafuata vifungu vya Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data (GDPR) ya Ulaya pamoja na sheria za sasa za kitaifa zinazotumika za uhifadhi wa data. Tafadhali soma taarifa hii ya faragha kwa makini kabla ya kuwasilisha ripoti.
Mhusika na anayewajibika kwa uhifadhi wa data:
Mhusika anayewajibika kwa ulinzi wa data ni:
ALDI Einkauf GmbH & Co. OHG
Eckenbergstraße 16
45307 Essen
Unaweza kuwasiliana na mhusika anayewajibika kwa uhifadhi wa data kwa barua pepe kupitia anwani ya datenschutz@aldi-nord.de na kwa kutuma barua kwa ALDI Einkauf GmbH & Co. OHG, z.Hd. Datenschutzbeauftragter, Eckenbergstraße 16, 45307 Essen.
Kusudi la mfumo wa utoaji siri, msingi wa kisheria na mtoa huduma
Mfumo wa utoaji siri mfumo wa (BKMS® System) unatumika kwa kupokea kwa usalama na kwa usiri, kuchakata na kudhibiti ripoti zinazohusu matukio ya ukiukaji wa kanuni za utiifu. Uchakataji wa data binafsi katika mfumo wa BKMS® System unalingana na maslahi ya kisheria ya kampuni yetu katika kugundua na kuzuia matumizi mabaya na kuepusha hasara kwa kampuni, wafanyakazi na wateja wake.
Mfumo wa utoaji siri unaendeshwa na kampuni maalum, EQS Group GmbH, Bayreuther Str. 35, 10789 Berlin Ujerumani, kwa niaba ya kampuni ya ALDI Einkauf.
Msingi wa kisheria wa uchakataji wa data binafsi ni Kifungu cha 6 aya ya 1 hoja ya f ya GDPR.
Uchakataji wa data binafsi
Data na maelezo binafsi yanayowasilishwa katika mfumo wa utoaji siri huhifadhiwa katika hifadhidata ya kituo cha data cha ulinzi wa juu kinachoendeshwa na EQS Group GmbH. Ni wafanyakazi wenye ujuzi na walioidhinishwa pekee wa kampuni ya ALDI Einkauf ndio wanaoruhusiwa kufikia data hiyo. EQS Group GmbH na washirika wengine hawawezi kufikia data hiyo. Hii inahakikishwa katika utaratibu ulioidhinishwa kupitia mbinu za kina za kiufundi na kishirika.
Data yote huhifadhiwa ikiwa imesimbwa kwa njia fiche kwa kutumia viwango vingi vya ulinzi wa nenosiri ili data iweze kufikiwa tu na idadi ndogo zaidi ya watu wenye ujuzi na walioidhinishwa moja kwa moja katika kampuni ya ALDI Einkauf.
Aina ya data binafsi inayokusanywa
Ni hiari yako kutumia mfumo wa utoaji siri. Ukiwasilisha ripoti kupitia mfumo wa utoaji siri, tunakusanya maelezo na data binafsi ifuatayo unayotoa:
- jina lako,
- unakofanya kazi, na
- majina na data nyingine binafsi ya watu unaowataja katika ripoti yako, ikiwa inahitajika.
Ushughulikiaji wa ripoti kwa usiri
Ripoti zinazowasilishwa hupokewa na idadi ndogo ya wafanyakazi maalum wenye ujuzi na walioidhinishwa moja kwa moja wa shirika la utiifu la ALDI Einkauf na hushughulikiwa kwa usiri kila wakati. Wafanyakazi wa shirika la utiifu la ALDI Einkauf hutathmini suala husika na kufanya uchunguzi zaidi unaohitajika kulingana na hali maalum.
Wakati wa uchakataji wa ripoti au wa kufanya uchunguzi maalum, huenda ikahitajika kutuma ripoti zilizowasilishwa kwa washirika wengine. Tutahakikisha kila wakati kuwa sheria zinazotumika za uhifadhi wa data zinafuatwa wakati wa kutuma ripoti.
Watu wote wanaoruhusiwa kufikia data husika wana jukumu la kudumisha usiri wa data hiyo.
Maelezo kuhusu mshukiwa
Tuna jukumu la kisheria la kufahamisha washukiwa kuhusu ripoti zozote zilizowasilishwa kuwahusu mara tu ufichuaji wa habari hizi hauhujumu tena uchunguzi. Utambulisho wako kama mtoboa siri, hata ukijitambulisha, kwa kawaida hautafichuliwa.
Haki zako
Kulingana na sheria ya uhifadhi wa data ya Ulaya, wewe na watu waliotajwa katika ripoti mna haki ya kufikia, kurekebisha, kufuta, kuzuia uchakataji na haki ya kukataa kuchakatwa kwa data yenu binafsi. Haki ya kukataa kuchakatwa kwa data binafsi ikitekelezwa, umuhimu wa data iliyohifadhiwa kwa uchunguzi wa ripoti utatathminiwa mara moja. Data ambayo haihitajiki tena itafutwa mara moja. Pia, una haki ya kukata rufaa kwa mamlaka ya usimamizi.
Kipindi cha kuhifadhiwa kwa data binafsi
Data binafsi itahifadhiwa mradi inahitajika ili kubainisha hali na kufanya utathmini wa mwisho au mradi kuna maslahi ya kisheria ya kampuni au ikiwa inahitajika kuhifadhiwa kisheria. Baada ya uchakataji wa ripoti kukamilika, data itaondolewa maelezo ya utambulisho na kufutwa kulingana na masharti ya kisheria.
Matumizi ya tovuti ya kutoboa siri
Mawasiliano kati ya kompyuta yako na mfumo wa utoaji siri hufanyika kupitia muunganisho uliosimbwa kwa njia fiche (SSL). Anwani yako ya IP haitahifadhiwa wakati unatumia mfumo wa utoaji siri. Ili kudumisha muunganisho kati ya kompyuta yako na mfumo wa BKMS® System, kidakuzi kilicho na kitambulisho cha kipindi pekee huhifadhiwa kwenye kompyuta yako (kinajulikana kama kidakuzi cha kipindi). Kidakuzi hiki hutumika tu hadi mwishoni wa kipindi na huacha kutumika unapofunga kivinjari chako.
Unaweza kusanidi kisanduku pokezi salama kinacholindwa na jina bandia / jina la mtumiaji na nenosiri ulilochagua mwenyewe ndani ya mfumo wa utoaji siri. Hii inakuruhusu utume ripoti kwa njia salama kwa kusema jina au bila kujitambulisha. Mfumo huu huhifadhi tu data ndani ya mfumo wa utoaji siri, hali inayofanya uwe salama hasa. Si namna ya mawasiliano ya kawaida ya barua pepe.
Kidokezo kuhusu kutuma viambatisho
Unapowasilisha ripoti au maelezo ya ziada, unaweza kuambatisha pia viambatisho. Iwapo ungependa kuwasilisha ripoti bila kujitambulisha, tafadhali fuata ushauri wa usalama ufuatao: faili zinaweza kuwa na data binafsi iliyojificha inayoweza kukutambulisha. Ondoa data hii kabla ya kutuma. Ikiwa huwezi kuondoa data hii au huna uhakika kuhusu jinsi ya kufanya hivyo, nakili maandishi ya kiambatisho chako kwenye ripoti yako au utume hati iliyochapishwa bila kujitambulisha kwa anwani iliyowekwa kwenye kijachini, ukitaja nambari ya marejeleo uliyopokea mwisho wa utaratibu.
Maelezo kuhusu uhifadhi wa data ya tovuti
Tafadhali pia soma maelezo ya uhifadhi wa data kwenye tovuti yetu:
https://www.aldi-nord.de/tools/datenschutzhinweis.html