Madhumuni ya ilani hii ya maelezo, kuhusiana na shughuli ya uchakataji iliyotajwa hapo awali, ni kukupa maelezo yote yanayohitajika na sheria zinazotumika na hasa yanayohitajika na Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data (“GDPR”).
Kitambulisho na anwani ya mawasiliano ya mdhibiti
Compagnie de Saint-Gobain
Saint-Gobain Tower, 12 place de l'Iris
92400 Courbevoie, Ufaransa
Anwani ya mawasiliano ya Ofisa wa Ulinzi wa Data (DPO)
Ili kutumia haki zako au iwapo una maswali yoyote kuhusu uchakataji wa data yako ndani ya mfumo huu, tafadhali tuma ombi lako kwa anwani ifuatayo: PrivacyContact.CSG.FR@saint-gobain.com
Madhumuni ya uchakataji wa data
Malengo:
Shughuli hii ya uchakataji imewekwa ili kuwezesha:
- Wafanyakazi na washirika wa nje na wasio wa kila wakati, kuripoti:
- kosa au matendo yasiyofaa;
- ukiukaji mkubwa na dhahiri wa ahadi za kimataifa zilizothibitishwa au kuidhinishwa ipasavyo na Ufaransa;
- ukiukaji mkubwa na dhahiri wa sheria mahususi ya shirika la kimataifa iliyotungwa kwa kuzingatia ahadi ya kimataifa iliyothibitishwa ipasavyo;
- ukiukaji mkubwa na dhahiri wa kanuni au sheria;
- hatari au madhara makubwa kwa maslahi ya umma ambayo yanafahamika kibinafsi na mtumaji wa ripoti;
- ukusanyaji wa ripoti kutoka kwa wafanyakazi wa Saint-Gobain Group kuhusiana na kuwepo kwa matendo au hali ambazo ni kinyume na Maadili ya Saint-Gobain Group na zinazoweza kuashiria ufisadi au uenezaji wa ushawishi.
- ukusanyaji wa ripoti zinazohusiana na kuwepo au kugunduliwa kwa hatari za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na haki za msingi, usalama na afya ya binadamu na mazingira, unaotokana na shughuli za huluki za Saint-Gobain Group, kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, pamoja na unaotokana na shughuli za wasambazaji au wakandarasi wadogo ambao wana uhusiano wa kibiashara na Saint-Gobain, wakati ambapo shughuli hizi zinahusiana na uhusiano huu;
- ukusanyaji wa ripoti zozote kuhusiana na tabia au hali yoyote ambayo ni kinyume na kanuni ya maadili ya Saint-Gobain Group.
Msingi wa kisheria wa uchakataji wa data:
Wajibu wa kisheria: uchakataji wa data ni muhimu kwa ajili ya kutii wajibu wa kisheria unaohitaji kutekelezwa kwa mfumo wa utoaji siri, hasa ule unaobainishwa kwenye Kifungu cha L. 225-102-4 cha Sheria ya Kiuchumi ya Ufaransa na Vifungu vya 17.II.2° na 8.III vya sheria ya “Sapin 2”.
Maslahi halali: uchakataji wa data huwezesha ukusanyaji wa ripoti zinazohusiana na shughuli za kujitolea zinazotekelezwa na huluki za Saint-Gobain Group (kanuni ya maadili ya ndani ya kampuni). Ripoti hutolewa kwa hiari ya wafanyakazi au wafanyakazi wa nje na wasio wa kila wakati.
Data na muda wa kuhifadhiwa.
- Ripoti isiyokubalika: bila kuchelewa
- Kufungwa kwa ajili ya kutokuwa sahihi au kamili: Miezi miwili baada ya kufungwa kwa shughuli zote za uthibitishaji au zinazokubalika
- Kufungwa kwa ajili ya utumiaji mbaya wa mfumo au kukosekana kwa ukweli wa kutegemewa: Kukamilika kwa kesi na/au kutolewa kwa adhabu
Panapofaa, watu hufahamishwa iwapo data inayohitajika ni ya lazima au isiyo ya lazima na athari wanazoweza kupata ikiwa watashindwa kujibu.
Wapokeaji
Data inayokusanywa inakusudiwa kutumiwa na watu wanaowajibika hasa kwa kudhibiti ripoti ndani ya huluki za Saint-Gobain Group na kutolewa kwa watu wengine (mawakili, wataalamu, wakaguzi wa mahesabu) kwa madhumuni ya kufanya uchunguzi na uchanganuzi.
Uhamishaji wa data nje ya Umoja wa Ulaya
Data iliyokusanywa inaweza kutolewa nje ya Umoja wa Ulaya, muradi hatua hii ni muhimu kabisa kwa ajili ya uchakataji wa ripoti zilizotumwa, hasa katika muktadha wa kufanya uchunguzi ili kuthibitisha ukweli kuhusu ukiukaji. Kabla ya uhamishaji wowote wa data binafsi, mdhibiti atahakikisha, hasa kwa kutumia Vifungu vya Kawaida vya Mikataba vya Tume ya Ulaya, kuwa watu wanaofikia data kama hiyo wanahakikisha kuwa watatoa ulinzi wa kutosha kwa data hiyo.
Haki za watu binafsi
Chini ya hali fulani, sheria zinaweza kukuruhusu utumie haki zifuatazo kuhusu data yako binafsi:
- Haki ya kufikia;
- Haki ya kurekebisha;
- Haki ya kufuta;
- Haki ya kuzuia uchakataji wa data;
- Haki ya kukataa;
Pia, una haki ya kuamua jinsi data yako itakavyoshughulikiwa baada ya kufariki.
Ikiwa unaamini, baada ya kuwasiliana nasi, kuwa haki zako haziheshimiwi au kuwa shughuli ya uchakataji wa data iliyobainishwa hapa ndani haitii kanuni za ulinzi wa data, una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka yako ya usimamizi.
Kuwasilisha ripoti kwa njia ya simu
Hali yako ya kutotajwa italindwa pia na mfumo wa BKMS® System unapowasilisha ripoti kwa njia ya simu. Saint-Gobain wala EQS Group haitaweza kupata nambari yako ya simu. Maelezo yako kuhusu tukio husika yatarekodiwa katika mfumo wa BKMS® System. Baadaye, faili ya sauti iliyosimbwa kwa njia fiche itanukuliwa na mfanyakazi anayehusika wa Saint-Gobain. Ikiwa umesanidi kisanduku pokezi salama baada ya kuwasilisha ripoti kwa njia ya simu, unaweza kupokea mwitiko kwa muundo wa rekodi ya sauti kutoka kwa mfanyakazi anayehusika wa Saint-Gobain, na unaweza kuongeza maelezo kwenye ripoti yako, ikiwa inahitajika. Pia, unaweza kufikia kisanduku pokezi salama kupitia programu ya wavuti, ukague mwitiko na uongeze maelezo ya ziada kwa muundo wa maandishi. Ili kulinda usiri wa ripoti yako au maelezo ya ziada, huwezi kuisikiliza kwenye simu yako wala kwenye kisanduku pokezi salama cha wavuti.
Maelezo ya ziada
Vipengele vya hati hii ya maelezo ya kina vinaweza kubadilika kulingana na masharti ya sheria za eneo zinazotumika.
Ili upate wakati wowote maelezo yanayohusiana na shughuli ya uchakataji wa data iliyotekelezwa, nenda kwenye ukurasa wa kwanza wa mfumo wa utoaji siri wa Saint-Gobain.
Unaweza pia kusoma Sera ya Faragha ya Saint-Gobain Group kwenye tovuti yetu ya shirika: www.saint-gobain.com.
Ilisasishwa mara mwisho tarehe : 27/06/2022