Utaratibu wa kuwasilisha ripoti ni upi? Ninawezaje kusanidi kisanduku pokezi?
Ili uwasilishe ripoti bila kujitambulisha au ripoti iliyowekewa mapendeleo, anza kwa kubofya kitufe cha “Wasilisha Ripoti“ kilicho katika sehemu ya juu kushoto ya ukurasa wetu wa habari.
Utaratibu wa kuripoti unajumuisha hatua nne:
- Kwanza, utatakiwa usome maelezo kuhusu jinsi ya kulinda hali yako ya kutotajwa kisha ujibu swali la usalama.
- Pili, utaombwa ueleze mada ya ripoti yako kwenye ukurasa unaofuata.
- Kwenye ukurasa wa ripoti, unaweza kufafanua ripoti yako kwa maneno yako mwenyewe na kujibu maswali kuhusu tukio husika kwa kuchagua tu majibu. Unaweza kuandika herufi zisizozidi 5,000 kwenye sehemu ya kuandika iliyowekwa, ambayo inalingana na ukurasa wa A4. Unaweza pia kuwasilisha faili isiyozidi MB 5 ya kuthibitisha ripoti yako. Tafadhali kumbuka kuwa hati zinaweza kuwa na maelezo kuhusu mwandishi. Baada ya kutuma ripoti yako, utapokea nambari ya marejeleo kama uthibitisho kuwa umewasilisha ripoti hiyo.
- Mwisho, utaombwa usanidi kisanduku pokezi salama chako binafsi kisicho na utambulisho. Kisanduku hiki pokezi salama kitatumika kuwasiliana nawe, kujibu maswali yako na kukupa taarifa kuhusu hali ya ripoti yako.
Iwapo tayari umesanidi kisanduku pokezi salama, bofya kitufe cha “Ingia” ili ukifikie moja kwa moja. Kwanza, utatakiwa kujibu swali la usalama.
Teknolojia inayotumika katika mfumo wa BKMS® System italinda hali yako ya kutotajwa mradi huwasilishi maelezo yoyote yaliyo na maelezo ya kukutambulisha.